SIKU YA KWANZA NILIPO INGIA MOCHWARI NILICHO KIONA NI NGUMU SANA KUELEZEA
Tuanzeee............. Kwanza niliona maneno yameandikwa (TULIKUWA KAMA WEWE). Kuelekea mlango wa kutokea niliona maneno yameandikwa (HIVI KARIBUNI UTAUNGANA NASI). Mh..! Kwa hakika niliogopa sana kuona miili ya watu ikiwa imelazwa katika sakafu pasipo kufunikwa kitu. Kulikuwa na maiti zaidi ya hamsini katika meza za kuoshea maiti,mingine ndani ya majokofu. Kulikuwa na miili ya watu wa jinsia zote.Tukasonga ndani zaidi kuelekea mahali ulipo hifadhiwa mwili wa rafiki yetu.Tulipoufikia mhudumu wa mortuary alifunua na ulikuwa haujavishwa nguo na umelazwa juu ya ubao. Nilimuangalia sana marehemu rafiki yetu akiwa amelala pale utupu,hakuweza hata kufunika utupu wake kwa mikono yake,wala kupinga chochote kile. Nikajiuliza sana NINI MAANA YA MAISHA? Kwanini tunatumia nguvu nyingi kutaka kumiliki kila kitu katika Dunia hii na wakati mwingine hata kwa kuwaumiza wengine? Kwanini tunakiburi,majivuno na ubinafsi kama tunaimiliki Dunia na pumzi ya uhai wetu? Kwanini hatuwezi hata kuwasam...