SIKU YA KWANZA NILIPO INGIA MOCHWARI NILICHO KIONA NI NGUMU SANA KUELEZEA
Tuanzeee.............
Kwanza niliona maneno yameandikwa (TULIKUWA KAMA WEWE).
Kuelekea mlango wa kutokea niliona maneno yameandikwa (HIVI KARIBUNI UTAUNGANA NASI).
Mh..! Kwa hakika niliogopa sana kuona miili ya watu ikiwa imelazwa katika sakafu pasipo kufunikwa kitu.
Kulikuwa na maiti zaidi ya hamsini katika meza za kuoshea maiti,mingine ndani ya majokofu.
Kulikuwa na miili ya watu wa jinsia zote.Tukasonga ndani zaidi kuelekea mahali ulipo hifadhiwa mwili wa rafiki yetu.Tulipoufikia mhudumu wa mortuary alifunua na ulikuwa haujavishwa nguo na umelazwa juu ya ubao.
Nilimuangalia sana marehemu rafiki yetu akiwa amelala pale utupu,hakuweza hata kufunika utupu wake kwa mikono yake,wala kupinga chochote kile.
Nikajiuliza sana NINI MAANA YA MAISHA?
Kwanini tunatumia nguvu nyingi kutaka kumiliki kila kitu katika Dunia hii na wakati mwingine hata kwa kuwaumiza wengine?
Kwanini tunakiburi,majivuno na ubinafsi kama tunaimiliki Dunia na pumzi ya uhai wetu?
Kwanini hatuwezi hata kuwasamehe watu wanaotukosea huku tukijihesabia haki kana kwamba sisi ni Malaika?
Kwanini hatuwezi hata kumkumbuka Muumba wa Mbingu na nchi tunapokuwa hai?
Niliona Matajiri waliokuwa na Majumba,waliokuwa na Degree na PhD,waliokuwa na Magari ya kifahari,waliokuwa Viongozi majasiri na mashupavu,mafukara na masikini,wanawake wazuri wenye mitindo mbalimbali ya nywele wote wakiwa wamelazwa humo ndani kimyaa kabisa.
Nikajisemea moyoni kumbe maisha sio kitu na niya muda tu,cheo ni cha muda,utajiri na heshima vyote nivya muda tu.
Sijui lini nitaondoka katika Dunia hii na nani watakuja kunizika lakini ninacho shukuru niliona vile nitakavyokuwa siku pumzi yangu itakapo ondolewa.
Ninatamani na kutaka kuwa bora zaidi ya jana yangu lakini si katika kushindana na watu au kuchukia watu bali unyenyekevu,kusamehe,kupenda na kujali wengine,kumuabudu Mungu na kumtumikia.
Nitajitahidi kaduri ya uwezo wangu kuwa mwema kwa kuwa maisha niliyonayo niya muda na tena kifo hakitazami status ya mtu.Naomba Mwenyezi Mungu unisamehe makosa yangu yote na unitangulie katika kila hatua ya majukumu yangu na maisha yangu pia.
📌
Ahsanteni
Comments
Post a Comment