Posts

Showing posts from September, 2024

KAMA UNADHANI KUNA KITU UNAFICHWA NA MATAJIRI, SAHAU KUHUSU UTAJIRI.

 nilisema kwamba "Ishara ya umasikini mbaya sio ule unaowakosesha watu pesa na mlo wa siku, ila ni ule unaowakosesha watu raha kwenye mafanikio ya wengine."  Tarehe 15/08/2024 saa 2:05 asubuhi nikasema tena "Kinachochelewesha maendeleo ya masikini wengi sio ugumu wa kupata pesa, ila ni ile tabia ya kupoteza muda kufuatilia maendeleo ya watu wengine." Na tarehe 17/08/2024 saa 3:21 asubuhi nilisema tena kwa nukuu mbili mfululizo kwamba   "Hatutofautiani vitu vingi na watu wanaofanya makubwa kwenye hii dunia, ila maarifa na taarifa tulizo nazo ndiyo zinazoamua tujione wa viwango gani na tunaelekea wapi kimaisha."  Na nukuu ya pili ilisema "Kama ambavyo nyanya moja mbovu huozesha tenga zima vikiwa pamoja, ndivyo ambavyo watu walioshindwa mambo mengi kwenye maisha yao hupambana kuwakatisha tamaa wengine." Nukuu hizo zinasadifu hoja mbalimbali ambazo watu wengi wamekuwa wakizitoa kwenye mahojiano ya matajiri wengi pindi wanaposema walianza na viwango f...