WAJUWE WAGOMBEA WA URAISI WA MAREKANI WALIO GOMBEA WAKIWA GEREZANI
DONALD TRUMP
Katika siku ambayo haijawahi kushuhudiwa katika siasa za Marekani, Donald Trump amekuwa rais wa kwanza mstaafu wa Marekani kupatikana na hatia ya uhalifu.
Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa huenda asitumikie kifungo kwa makosa 34 ambayo amepatikana na hatia katika hukumu itakayo tolewa siku ya Alhamisi katika chumba cha mahakama cha Manhattan.
Bado ana uwezo wa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo - mchakato ambao pengine utaendelea hadi uchaguzi wa Novemba au zaidi.
Hata kama hukumu itathibitishwa, huenda akapigwa faini, au akawekwa katika kipindi cha uangalizi. Lakini hata ikiwa atakwenda jela - Trump anaweza kuendelea kuwa mgombea na uwezekano wa kuwa rais wa Marekani akiwa jela.Matakwa ya kisheria kwa wagombea urais hayajabadilika tangu 1789, mwaka ambapo George Washington akiwa rais wa kwanza wa Marekani.
"Sifa ya kuwa mgombea ni lazima awe umezaliwa Marekani au katika maeneo yake. Na anapaswa kuwa na umri fulani ambao ni kuanzia umri wa miaka 35,” anasema Prof Iwan Morgan, profesa mstaafu wa historia ya Marekani katika Chuo Kikuu cha London.
Mgombea pia awe amekaa Marekani kwa miaka 14 – takwa lililowekwa baada ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe ili kuwazuia watu ambao waliasi dhidi ya Marekani," anasema Prof Morgan.
Lakini hakuna marufuku kwa wahalifu waliopatikana na hatia kugombea Ikulu ya White House. Na kuna sababu ya kihistoria katika hilo.
"Marekani ilizaliwa kutokana na mapinduzi, na kulikuwa na uwezekano kwamba mtu ambaye aliwekwa gerezani kwa kupinga ufalme - Marekani ilipokuwa koloni la Uingereza - angeweza kuondolewa kuwania urais."
“hakuna hata mmoja miongoni mwa waanzilishi wa mkataba ambao uliunda katiba ya Marekani mwaka 1787 - waliofungwa na Waingereza, lakini wengine walikaribia kufungwa," anasema Prof Morgan.
"Kama mapinduzi yasingefaulu, wangekuwa na hatia ya uhaini dhidi ya ufalme, na wangekuwa wahalifu."
EUGENE V DEBS'S
Hii ndiyo sababu waandishi wa katiba hawakutaka kuweka vikwazo juu ya nani anaweza kuwa rais. Na sera imesababisha wagombea watatu kufanya kampeni za urais wakiwa ndani ya gereza.Eugene V Debs's aligombea uraisi 1912 na 1920 kipindi cha mafanikio makubwa kwa ujamaa Marekani
"Mgombea aliyegombea nafasi ya urais akiwa katika gereza la serikali alikuwa Eugene Debs mwaka 1920," anasema Prof Morgan.
Debs alikuwa gerezani kwa mara ya kwanza mwaka 1894. Kama afisa wa chama cha wafanyakazi aliongoza upinzani dhidi ya kampuni ya treni, alipatikana na hatia ya kuzuia barua za posta.
Jeshi lilivunja mgomo huo na Debs akaenda jela kwa miezi sita.
“Mapema katika Karne ya 20, akawa mwanachama wa Chama cha Kisoshalisti cha Marekani. Aligombea urais 1904, 1908, 1912 na 1920,” Prof Morgan anaeleza (Debs pia aligombea kwa tiketi ya Social Democratic Party mwaka 1900).
"Mwaka 1912, katika kinyang'anyiro cha wagombea wa nne kilichohusisha Democrat, Woodrow Wilson, Republican, William Howard Taft, mgombea wa Progressive na Rais wa zamani wa Republican Theodore Roosevelt, na Debs ambaye alifanya vyema sana."
Alipata karibu kura milioni moja, 6% ya kura zote, "asilimia kubwa zaidi kuwahi kushinda mgombea wa Chama cha Kisoshalisti huko Marekani."
Lakini wakati wa vita vya Kwanza vya Dunia. Debs alipinga vita na kuwashawishi Wamarekani wasishiriki katika vita.
"Mapema wakati wa msimu wa vuli wa 1918 - vita vilikuwa karibu kwisha wakati huo - alitoa hotuba huko Canton, Ohio, aliwahimiza Wamarekani kupinga kuandikishwa jeshini," anasema Prof Morgan.
Debs alishtakiwa kwa uchochezi na kupelekwa gerezani katika Gereza la Shirikisho la Atlanta Aprili 1919. Bado alikuwa katika gereza hilo wakati wa uchaguzi mwaka uliofuata, na Chama cha Kisoshalisti cha Marekani kilimteua kuwa mgombea wao.
Debs alishinda kura nyingi zaidi kuliko alizopata mwaka 1912 (kura 914,191 mwaka 1920 na 901,551 mwaka 1912). Lakini wakati huu alipata 3% tu ya kura zote, baada ya wanawake kuruhusiwa kupiga kura.
Aliachiliwa baada ya kutumikia karibu miaka mitatu gerezani, lakini afya yake haikupata nafuu na alikufa mwaka 1926.
Comments
Post a Comment