Kuajiriwa ni utumwa?
Karibu kweny makala hii ya jifunzekitu natumaini wewe ni mzima wa afya kabisa karibu tuanze madaaaa..
Vitu vya kukuingizia kipato huwezi kuvijua na kuvifanya kwa kuvisoma tu hata wakikupa vitabu 1,000 au ukiangalia video 10,000. Kusoma sawa inakupa "basics" au msingi lakini lazima uanze kuvifanya "on job training" na "performance"
Ule msemo "experience is the best teacher" ni ukweli 💯. Hata kama hutaki kukosea basi uwe pembeni ya mtu anayefanya hicho kitu bega kwa bega, mguu kwa mguu kama mapacha walioungana. Na bado usipofanya kuna mahali utakwama tu!
Ukichunguza utagundua wafanyabiashara wenye maduka Ilala au Mwenge walikuwa wameajiriwa maduka ya kariakoo. Iwe ni kuuza "spare" za magari au nguo. Wenye "clinics" nyingi mtaani walikuwa wameajiriwa Muhimbili au Mwananyamala!
Hii ina maana kubwa sana kwamba usidharau ajira hata kidogo. Hata kama una mshahara kidogo heshimu sana kazi yako na mheshimu sana mwajiri wako. Tena kuwa karibu naye uone anafanya nini usiishi kizembe!
Nakuambia haya kwa sababu miaka michache ijayo huwezi kupata hiyo fursa ya kujifunza hata kama una "boss". Kwa sababu dunia ya Ai na Robots haihitaji "mwajiri wako" kufanya kitu zinafanya "robots" na Ai.
Utajifunza vipi? "On job training"? Maarifa yote ya biashara "Boss" wako anaifundisha "robot" tunaita "machine learning". Ndio itakuwa inapata "on job training" sio wewe! Tena nchi nyingi tayari, Tz ipe miaka 2 utanikumbuka!
Anayekuambia kuajiriwa ni utumwa hana uzoefu wa biashara na bado hajakomaa kwenye masuala ya "career". Ajira inakufundisha misingi na mifumo "systems". Inakujengea "nidhamu". Inakupa "network" na inakupa "Mentorship"
Ndio maana mfanyabiashara mzuri ni yule ambaye anajua ameajiriwa na "mteja". Ndio maana ya "Mteja ni Mfalme". Anayempa mfanyabiashara "on job training" ni mteja! Hakuna somo kubwa kama kumpoteza mteja. Wanaofanya biashara wananielewa!
Ina maana kama hauwezi kuheshimu kuajiriwa na kumheshimu aliyekuajiri unasema "unamtajirisha" au "ni mnyonyaji", ni ngumu sana kufanya biashara. Mwajiri wako ni mteja wako na wewe ni mteja wa mwajiri wako kama mteja utakaye kuwa nae ukijiajiri mwenyewe!
Na kama unateseka, jifunze, pata "network" uondoke! Kama umekuwa mkubwa kiasi kwamba mwajiri wako hawezi kukidhi thamani yako na mshahara, jenga Cv yako ondoka! Lakini hicho ulichokipata hapo sio kitu kidogo usikidharau..ni "biashara" Academy!
Kwahiyo kuajiriwa ni baraka sio utumwa! Acha kumpa "mwajiri" wako majina; "shetani" kimeo nk. Utumwa ni kukosa "growth mindset". Kama unawaza mbali changamoto za ajira ni mapito tu ya muda. Na kama huwezi changamoto za ajira basi usijaribu biashara utakufa.
Comments
Post a Comment