SABABU INAYO KUFANYA URUDI NYUMA KIMAFANIKIO KILA SIKU HIZI HAPA
wakati inatokea mambo yako yanaenda vizuri, ghafla changomoto inatokea na kukurudisha nyuma kabisa.
Je, ulishawahi kujiuliza kwa nini hali hiyo inatokea kwako, na pengine wapi unakosea sana hadi iwe hivyo kwako wewe?
Kwa mfano, utakuta kipato chako kinaanza kukua, ila kuna jambo linajitokeza na unajikuta unatumia pesa zote.
Unakuta ni kweli umeanza mahusiano yako mapya vizuri, lakini ghafla kuna kitu kinaingilia na kuharibu mahusiano hayo.
Unakuta umeanza biashara yako vizuri, lakini ghafla zinatokea changamoto ambazo zinaharibu kabisa biashara hiyo na kuiua.
Kuna wakati unakuwa una waza una mkosi? lakini unachotakiwa kujua upo kwenye changamoto inayosababishwa na wewe.
Hakuna mkosi wala laana uliyonayo, unatakiwa ujichunguze ni wapi unakosea sana hadi iwe hivyo kwako.
Kama usipojipa umakini wa kujichunguza na kuangalia hasa sababu ni nini, basi utaishia kukwama hapo hapo.Usitafute mchawi, tatizo na chanzo kikubwa ni wewe, angalia ni wapi unakosea na kisha jirekebishe, songa mbele.
Comments
Post a Comment