Tatizo linalokumba watu wengi

Moja kati ya tatizo kubwa ambalo huwakumba watu wengi hususani suala kuanzisha biashara ni pamoja na kufikiria kuanzisha biashara hizo wakiwa na mitaji mikubwa sana.


Unakuta mtu uwezo wake ni mdogo, ila hana uwezo wa kulitimiza wazo hilo mwisho wa siku mtu huyu anaacha kabisa kufanya au kutimiza wazo hilo kwa sababu uwezo wake ni mdogo. Idadi ya watu ambao huwa wanakumbwa na tatizo hili ni wengi sana.


Hivyo ninachotaka kukuambia siku ya leo ni kwamba usiogope kuanzisha biashara au jambo fulani kwa sababu ya ukubwa wa mtaji wa kuanzisha jambo hilo bali unachopaswa kuelewa ni kwamba, kila kitu ambacho unakiona leo hii katika ukubwa fulani kumbuka kitu hicho kilianza na hatua ya chini sana.


Kama unataka kuanza kufanya jambo fulani basi ni vyema ukaanzia hapo ulipo na pia anza na kile ulichonacho, kwa sababu kama huwezi kuanza kwa hatua ndogo, basi huwezi kufikia hatua kubwa zile ambazo unazitaka.

END

     ASANTE SANA KWA MDA WAKO MUNGU AKUBARIKI 🙏🙏

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kumfanya mwenzi wako akupende zaidi kwa limbwata rahisi tu

NAMNA YA UMASIKINI UNAVYOTENGEZWA

NJIA ZA KUWA NA MAFANIKIO KATIKA MAISHA