Usomaji nyota Aliamisi 11/4/2024


SAMAKI


Umelindwa sana dhidi ya hali zozote mbaya na watu wabaya. Je, unatarajia mazuri kutoka kwa watu ambao wamekuwa wakikutendea vibaya? Hao hawana nia yoyote nzuri kutoka kwako, wanahitaji tu kitu kutoka kwako. Mtu atakiri kitu kwako akiwa amelewa, nadhani mtu huyu amekuwa na wewe kwa miezi. Mtu ambaye aliondoka kutoka kwako tangu mwezi wa tano (May) mwaka jana anarudi mwezi huu wa tano unaokuja. 


NDOO


Usiruhusu mtu yeyote au kitu chochote kikuwekee kikomo au kikuzuie. Ulizaliwa kuwa mkuu. Ni wakati wa kuingia katika uwezo wako. Ondoa mawazo yako kichwani, acha kuruhusu wengine wakuambie kile unachoweza kufanya, inuka na ufanye una uwezo wa kufanya chochote. Unaongozwa kuelekea kwenye mabadiliko ya maisha. Yatakuwa makubwa na mazuri. 


MBUZI


Nahitaji kukukumbusha kwamba kwa vile ni vizuri kuwa na watu karibu nawe, familia, marafiki. Mtu muhimu zaidi katika maisha yako ni wewe mwenyewe. Jilinde kwa gharama zote. Kamwe usijidhuru we mwenyewe kwa kujaribu kuokoa wengine.


MSHALE


Nataka tu kukukumbusha jinsi ulivyo na akili, uwezo na mzuri vile vile. Hivi majuzi umesahau tu jinsi ulivyo mkuu. Umekuwa na siku chache ngumu na mawazo mabaya au kukataliwa. Itaisha hivi karibuni. Unahisi kukwama lakini mambo yataimarika hivi karibuni.


NG'E


Kukutana na watu wapya, kutengeneza urafiki mpya. Mradi mpya wa ubunifu na marafiki pia, kuwa mwangalifu na kuharibu mambo na urafiki na biashara. Unahitaji kupata miwani mipya. Kununua maua au mimea ya kupamba nyumba yako. Uwazi unakuja kuhusiana na nia ya mtu, hasa ikiwa hii ni kuhusiana na mfanyakazi mwenzako, unaweza kugundua kitu kuhusu yeye. 


MIZANI


Uwe na shukrani kwa yote uliyonayo. Roho (spirit) inakuhimiza kuwa na shukrani kwa wingi na baraka unazopokea. Hiyo ndio njia bora ya kuhakikisha kuwa mambo mazuri yanaendelea kuja kwako. Watu wenye shukrani wana furaha zaidi, hawana stress, na wanaridhika zaidi na maisha yao. Kuwa tayari kupokea. Kushukuru ni mchakato mzuri wa kuhamasisha nguvu zako na kuleta zaidi ya kile unachotaka katika maisha yako.


MASHUKE


Ndio unapaswa kuanza kubuni na kushona nguo zako za zamani. Uaminifu utakuokoa, ikiwa muongo utagundulika haraka. Urafiki mpya unakuja. Umechoka sana, kiroho, kifedha na kila kitu. Umechoka kutoka ndani ya moyo wako na watu wanaendelea kukujaribu. Watu wamekuwa wakikuchokoza na umechoka sana. Siku mbaya haimaanishi kuwa maisha ni mabaya. 


SIMBA


Umekuwa hoi sana hivi majuzi. Ikiwa ungejiruhusu kuhisi kila kitu kinachoendelea kwako, ungevunjika kabisa na usifanye chochote. Umechoka sana. Mzigo ni mzito sana, kifedha, kihisia na kila kitu. Umechoka. 


KAA


Una busara kuliko unavyokubali kuwa, tumaini hisia zako. Kitu kilitokea. Tukio ambalo mtu alikukosea. Mtu ambaye ni muhimu kwako amekukatisha tamaa (amekulet down). Hivi karibuni imekuwa ni vigumu sana kuamka kutoka kitandani, kwenda kazini, kutafuta kazi, kula, kulala. Amini kuwa utashinda yote hayo, nakuhakikishia. Mafanikio yapo yanakuja.


MAPACHA


Utapokea heshima na kutambuliwa kutoka kwa wale walio karibu nawe. Unafanya vizuri na unaendelea vizuri ondoa shaka. Umekuwa na mawazo na wasiwasi kwa kila jambo. Wakati fulani unahisi kama uko nyuma kwa kila kitu. Unahisi kama haujafanikiwa vya kutosha lakini mengi mazuri yatatokea kwa muda mfupi tu. Pumua! 


NG'OMBE


Kuondoa stress na wasiwasi kwa kutumia muda kutoka out. Rangi mpya kwenye nywele zako kwa baadhi yenu. Hutofulia tena miezi michache ijayo. Kuna fursa nyingi za kupata pesa na zitakuwa hazikutarajiwa. Itakushangaza maana huelewi jinsi ulivyo mkuu.


PUNDA 


Utaonekana vizuri ukiwa na nywele fupi. Samaki anakupenda lakini hatofanya juhudi kuja kwako. Mipango mipya na wapendwa wako inakuja, labda hautotaka kwenda na kujisikia uvivu kuhusu hilo lakini wataheshimu hilo. Ikiwa una hisia za kuelekea kwa rafiki yako wa karibu, nadhani ni jambo sahihi. Mtu ambaye ni mkubwa kwako anatazamia au ana nia ya kukufanya ujisikie vibaya kwa sababu ana wivu na anamaanisha kweli. Tarajia mabadiliko fulani kuhusu mazingira ya familia yako. 


Hizi ni jumbe za jumla hivyo haziwezi kumhusu kila mtu kwa kila kinachotabiriwa hapa. Chukua kile kitakachokuhusu na uache ambacho hakikuhusu kitamhusu mwingine usilazimishe ujumbe ambao sio wa kwako utashindwa kuelewa!

ASANTE KWA MUDA WAKO ENDELEA KUFUATILIA KWA USOMAJI WA NYOTA KILA SIKU 

   

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kumfanya mwenzi wako akupende zaidi kwa limbwata rahisi tu

NAMNA YA UMASIKINI UNAVYOTENGEZWA

NJIA ZA KUWA NA MAFANIKIO KATIKA MAISHA