Utabiri wa nyota Aliamisi 18/4/2024
USOMAJI NYOTA ALHAMISI 18/4/2024
MBUZI
Mtu anajuta kukutupa mbali, anaweza kuwa anarudi. Usiwaze kuhusu siku zijazo, usiwaze katika kichwa chako kuhusu hilo! Kila kitu kitageuka kuwa cha kushangaza. Hivi karibuni utapata msamaha huo kutoka kwa mtu wako. Pesa nyingi zitaingia (July). Maisha ya anasa. Mtu anafikiria kuwa umemkasirikia ndiomana anajishtukia. Kumuokoa mnyama.
NDOO
Mtu atalipia kutengeneza kucha zako. Kurejeshewa (refund) kitu. Kuona rangi halisi za mtu kazini. Kupandishwa cheo na kuwa kiongozi wa zamu. Kupatana na ex wako, na kumpa nafasi ya mwisho. Video yako kusambaa mbali kwenye TikTok. Mazuri zaidi bado yanakuja. Kupanuka katika maisha yako, hakuna tena kukwama katika sehemu moja, kueneza mbawa zako yaani kujiachia. Milango mipya inafunguliwa mwezi May. Barabara ya utajiri. Kuona 777.
SAMAKI
Chochote unachokihairisha kifanye! Kupata unafuu mwingi juu ya hali yako ya kifedha. Kuumiza kichwa wakati mtu wako anafikiria kupita kiasi kuhusu wewe. Kujisikia kama wewe tena, au kama toleo lako bora zaidi wewe mwenyewe, hakuna tena kujisikia uko chini. Mtu hazuii tena hisia zake kwako, tarajia kufungukiwa na mtu huyu, mambo yatakwenda haraka.
PUNDA
Kuona biashara yako ikivuma. Mzigo au kifurushi chako kitachelewa kuwasili. Kupata kuangaliziwa bure mambo yako kwa mtaalamu wa nyota. Toka nje zaidi utajisikia vizuri. Unahitaji kupumzika na kuchaji upya. Weka nafasi ya kupumzika. Habari njema kuhusiana na biashara inayohusu mawasiliano. Kupata uwazi juu ya maisha yako ya mapenzi.
NG'OMBE
Kuhisi huzuni juu ya siku za nyuma. Mtu anakulaghai (anakutapeli). Kushinda kesi mahakamani. Mtu anakupa pesa. Kupata maumivu ya tumbo. Mtu atafanya kazi kwa muda wa ziada ili kurejesha uaminifu wake. Nia za kweli za mtu zitaonyeshwa wazi zaidi! Hakuna mashaka tena. Kutengeneza pesa kutokana uundaji wa maudhui (content).
MAPACHA
Kuanzisha utaratibu mpya kwenye mazoezi (gym) unaokupa matokeo ya kushangaza. Tumbo kujisikia kuuma? Unakula vyakula ambavyo tumbo lako linashindwa kuvumilia? Sikiliza mwili wako zaidi. Umepata kazi tayari, tarajia simu ndani ya siku 1-9 zinazofuata. Kuzingatia kile unachotaka na mipango yako ya muda mrefu. Kutoka out kula ice cream. Mahojiano (interview) au usaili unaendelea vizuri, au kupigiwa simu kutoka huko.
KAA
Kudondosha simu yako majini. Kusikia majibu kutoka kwenye maombi yako ya kazi uliyotuma. Kualikwa kwenye harusi au baby shower ya mtoto. Kutengeneza pesa, biashara yako ya mtandaoni kuanza kuchanua. Kusikia au kumuona mmoja wa viongozi wako wa kiroho (mzimu, ruhani, au malaika). Mtu atakupa sh 250000 ya kitanzania.
SIMBA
Kuona mtoto wako akichukua hatua za kwanza (kuanza kuongea au kuanza kutembea). Kujifunza kuhusu nia ya kweli ya mtu. Rafiki anakuja kwako. Kushinda zawadi. Kupigana na mfanyakazi mwenzako. Kupata nafasi mpya ya kazi. Kusafiri nje ya nchi. Kupasuka kwa tairi. Kubadilishiwa oil bure (kwa wale wenye chombo cha moto).
MASHUKE
Kufanya kazi nyingi kwa dakika za mwisho. Kushinda pesa. Kuhisi kuishiwa nguvu. Kuhamia katika nyumba mpya. Kugombana na wazazi wako. Kucheza kwenye onyesho (show). Kuona malaika namba 222 mara nyingi zaidi. Uponyaji kutoka kwenye mshtuko wa moyo (heartbreak). Kuwa mpenzi wa mtu. Kukuza mapenzi kwa mtu darasani kwako (huyu ni crush wako).
MIZANI
Kuwa na ujasiri zaidi linapokuja suala la mwonekano wako. Kupata ukweli kuhusu nia ya mtu. Profesa wako wa chuoni atatoa mfano kutoka kwako ambao unaweza kuwa mzuri au mbaya. Kupata kitu bure. Pesa zako zikirudishwa mara kumi baada ya kuamua kumbariki mtu. Kukutana na rafiki ambaye haukumtarajia lakini ni mpya.
NG'E
Kuvunja kitu, inaweza kuwa sahani au kikombe cha udongo? Kusikia majibu kutoka kwa mtu ambaye hukuwasiliana naye. Kudhihirisha (manifesting) yaani kupata gari jipya au nyumba mpya. Kukutana na mwenza wa roho yako (soulmate). Kugombana na ndugu juu ya kitu kidogo. Kupata pesa zaidi kwenye tips.
MSHALE
Maumivu ya sikio au maambukizi ya kwenye sikio. Dhihirisho (manifestations) au haja ya pesa inakuja kwa nguvu. Kuachana na mambo ya nyuma na kupata njia ya kusonga mbele. Wakati zaidi wa kujijali we mwenyewe. Mtu atawasiliana nawe pasipo kutegemea, hukutarajia kusikia kutoka kwake. Mtu atakununulia kitu. Kupokea zawadi. Machozi ya furaha, kujisikia kukamilika. Kutendewa kitu kizuri. Kupiga hatua bila kutarajia.
Hizi ni jumbe za jumla hivyo haziwezi kumhusu kila mtu kwa kila kinachotabiriwa hapa! Chukua kile kitakachokuhusu na uache ambacho hakikuhusu usilazimishe ujumbe ambao sio wa kwako utashindwa kuelewa!
Comments
Post a Comment