Utabiri wa nyota jamatatu tarehe 15/4/2024


USOMAJI NYOTA JUMATATU 15/4/2024 


PUNDA


Kadri unapoendelea kujichagua we mwenyewe na kujiweka sawa kimaisha na kuanza uponyaji, huyu ex ambaye anaweza kuwa ni mwenye nyota ya Ndoo atajaribu kurudi. Unaweza kuzungumza kama marafiki ikiwa unataka, lakini usije kuanguka au kunasa kwa maneno yake.


NG'OMBE


Najua umekuwa mchovu sana hivi majuzi na unahisi kuvunjika moyo. Nahitaji ujue kuwa ni zamu yako inayokuja sasa kuwa na furaha. Ni wakati wa wewe kuwa na furaha, utulivu wa kifedha, katika mapenzi na udhibiti wa maisha yako na siku zijazo.


MAPACHA


Pindi unapohitaji kufanya kitu muhimu, chochote ambacho kinaweza kwenda vibaya, kinaenda vibaya siku ambayo unahitaji amani kufanya kitu muhimu. Mtu anakuombea anguko lako wiki hii, ana mipango mibaya dhidi yako. Endelea kuombewa upate ulinzi. Una mtu wa zamani anayerudi. Lakini unaonywa usipoteze kile unachohitaji kufanya. Una mambo ambayo unapaswa kufanya na kuzingatia kwa sasa. Umefika mbali sana na maisha yako na huhitaji kuwa na vikwazo vyovyote. Ni wakati wa kujikusanya pamoja. Wiki na miezi hii michache iliyopita inaweza kuwa ngumu kwako. Naona mambo yataanza kukuendea vizuri. Kuwa pale ambapo amani itakuwepo. Hilo ni muhimu kwako wiki hii.


KAA


Siku mbaya au wiki mbaya haimaanishi kuwa maisha yote ni mabaya. Mambo yamekuwa magumu na imekuwa ngumu kuona mwanga wa kule unakokwenda, lakini upo usikate tamaa. Na pindi utakapoona kile kizuri kilichohifadhiwa kwa ajili yako, utakuwa na furaha zaidi kupitiliza. 


SIMBA


Baraka inakuja kwako ili kukukomboa kutoka kwenye hali ngumu. Ninaona wapenzi/wachumba wengi wakivutiwa nawe. Kuwa mwangalifu kuungana tena au kupatana na mtu yeyote kwa wakati huu. Kiukweli ninahisi kama mtu huyu harudi kwa kheri au aina fulani ya kulipiza kisasi kwa kitu ambacho kilifanyika katika siku za nyuma. Ikiwa umepofushwa na hili, jua tu mwisho wa uhusiano kati ya mtu ambaye ulifikiri unaweza kumwamini unakuja kuwa mwisho. Ninaona pia utajifunza kitu muhimu kutokana na hili.


MASHUKE


Mambo yamekuwa magumu kidogo lakini wiki hii inakuja na pesa nyingi na shughuli za kufurahisha. Umekuwa chini kwa muda na kujisikia kukwama. Kuna kitu kizuri kinakuja kukukumbusha kuwa wewe sio wa kuishiwa hivyo. Daima umekuwa mpambanaji.


MIZANI


Mtu kichwani kwake anafikiria kuhusu wewe. Hujafanya chochote kibaya wacha kujipa presha. Kukuza uhusiano na mtu unayemjali, lakini labda amekuwa akikuweka mbali. Nyakati ngumu zinaisha. Acha kujidharau mwenyewe na wale wanaokuopenda! 


NG'E hii itakuwa nzuri kwako, haswa jumatano. Utapokea habari njema kuhusu stress kubwa uliyokuwa nayo. Labda mahojiano (interview) ya kazi unayotaka au mipango fulani ya kipesa. Baada ya hali ya kudorora uliyokuwa nayo, matumaini yako yatarejeshwa wiki hii.


MSHALE


Mtu wako wa zamani ambaye anaweza kuwa ni mwenye nyota ya Ndoo atakuja na kuomba msamaha kwa jinsi alivyokutendea huko nyuma. Msamaha ni wa dhati lakini hakutakuwa na kujitolea au ahadi yoyote mwanzoni. Kila mtu aliyekuumiza anapata anachostahili, karma. Habari njema kuhusiana na mtu unayemtazama kwa kumtamani na anakuchanganya. Kupokea kiasi cha pesa za ziada kutoka kwa familia/wapendwa wako.


MBUZI


Kujipenda na kujifunza kuweka mipaka kwa watu ambao wanaenda kinyume na wewe au kukufanya usijisikie huru. Baadhi ya mabadiliko katika mwonekano wako pia, rangi mpya ya nywele? Kukata nywele au kutaka tu kuonekana tofauti ili kuanza sura mpya. Baadhi ya matatizo ya gari/simu yako kutatuliwa. Unaepuka gharama zisizotarajiwa na kutumia pesa zako kwa hekima.


NDOO


Tarajia aina fulani ya msamaha kuja kabla ya msimu wa masika haujaisha kwa baadhi yenu. Baadhi yenu mko tayari kurekebisha kile kilichokuwa kimevunjwa, lakini kwa wengine hamtaki kusikia hata kidogo. 


SAMAKI 


Mtu ambaye umekatisha muunganisho naye kwa masharti mabaya anataka kukuomba msamaha. Ninahisi kama muda ambao atakaorudi tayari utakuwa umetulia kwa furaha na mtu wako halisi yaani mtu wako mpya. Kujifunza kitu kipya. Kujua kitu kuhusu mtu fulani. Kutokuwa tegemezi tena. Kujichagua mwenyewe, kujipenda. Kukutana na mtu mpya. 777.


Hizi ni jumbe hivyo haziwezi kumhusu kila mtu kwa kila kinachotabiriwa hapa! Chukua kile kitakachokuhusu na uache ambacho hakikuhusu usilazimishe ujumbe ambao sio wa kwako utashindwa kuelewa

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya kumfanya mwenzi wako akupende zaidi kwa limbwata rahisi tu

NAMNA YA UMASIKINI UNAVYOTENGEZWA

WAJUWE WAGOMBEA WA URAISI WA MAREKANI WALIO GOMBEA WAKIWA GEREZANI