SIFA ZA MALENGO
1 Yawe wazi yaani yaweze kueleweka kwa wepesi
2. Malengo yanatakiwa kuandikwa
-Usiweke malengo kichwani peke yake fanya kuandika malengo yako..
3. Yawe na uhalisia
- Usiweke malengo nje ya uhalisia.
-Usiweke malengo ya mauzo ya 100M kwa mataji wa 10K.
4. Yaweze kupimika
-Usiweke malengo ambayo hayawezi kupimika kwa mda husika.
5. Malengo yategemee na hali ya sasa.
- Usiweke malengo nje ya uhakisia wako wa sasa.
6. Yawe na mda maalumu.
- Usiweke malengo yasiyo na mda maalumu. Inaweza kuwa mwaka/mwezi.
7. Weka malengo ambayo yanaweza kutekelezeka.
- Usiweke malengo magumu sana mpka unaogopa kutekeleza.
8. Malengo hayatakiwi kuwa mengi mpka yakuvuruge.
- Utakuta mtu ana malengo mengi mpaka yana mvuruga.
9. Jitaidi malengo yako yakite sehemu nyeti kwenye biashara yak.
- Mfano sasa unataka ufike mauzo ya (3,000,000) kwa mwezi (3M) je utafanyaje?
- Tumia mbinu- Zingatia kanuni 80/20 rule
- Gawanya mauzo 3M kwa siku 30 kwa siku ni mauzo ya 100,000 (Laki moja)
- Gawanya laki 1 kwa masaa ya kazi kwenye biashara yako.
Mfano: msaa ya kazi yakiwa 12 basi utahitajika kuuza 8,500 kwa saa...
Tambua idadi ya wateja wako ambao wanaweza kufika hayo mauzo kwa siku.
- Usifanye biashara mpaka ufike mauzo yako kwa siku
-fanya hivyo kila siku bila kuchoka kanuni ya 80/20 rule inasema hivi
80% ya mauzo ya laki moja yanatakiwa yatokee kwenye 20% ya wateja
Mfn; Ikiwa wateja 10 wanaweza kukupa mauzo ya laki kwa siku basi kanuni ya 80/20 itakuwa hivi - wateja 2 waweze kukupa 80,000/=
Kwenye biashara unatakiwa kuzingatia wateja wenye hela nyingi kwa wingi usisahau kuweka malengo yako sawa sawa.
Comments
Post a Comment