WAJUWE WAGOMBEA WA URAISI WA MAREKANI WALIO GOMBEA WAKIWA GEREZANI
DONALD TRUMP Katika siku ambayo haijawahi kushuhudiwa katika siasa za Marekani, Donald Trump amekuwa rais wa kwanza mstaafu wa Marekani kupatikana na hatia ya uhalifu. Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa huenda asitumikie kifungo kwa makosa 34 ambayo amepatikana na hatia katika hukumu itakayo tolewa siku ya Alhamisi katika chumba cha mahakama cha Manhattan. Bado ana uwezo wa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo - mchakato ambao pengine utaendelea hadi uchaguzi wa Novemba au zaidi. Hata kama hukumu itathibitishwa, huenda akapigwa faini, au akawekwa katika kipindi cha uangalizi. Lakini hata ikiwa atakwenda jela - Trump anaweza kuendelea kuwa mgombea na uwezekano wa kuwa rais wa Marekani akiwa jela.Matakwa ya kisheria kwa wagombea urais hayajabadilika tangu 1789, mwaka ambapo George Washington akiwa rais wa kwanza wa Marekani. "Sifa ya kuwa mgombea ni lazima awe umezaliwa Marekani au katika maeneo yake. Na anapaswa kuwa na umri fulani ambao ni kuanzia umri wa miaka 35,...